Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni ...
Suala la ndoa ya Imamu Husein (a.s) na bibi Shahre Baanu aliyetekwa na jeshi la Kiisalamu, ni suala liliozungumziwa na vitabu vya historia huku likiwa na rangi mbali mbali za Ibara zenye kutofautiana, baadhi ya kauli zimesema kuwa: yeye alitekwa katika zama za utawala wa Omar, huku ...
Sisi swali lako tumelifanyia utafiti, na kulisaka katika maandiko mbali mbali yanayoelezea msiba wa Imamu Husein (a.s), vile vile tumeangalia ndani ya kitabu maarufu kijulikanachoa kwa jina la Luhuuf cha Sayyid Ibnu Taawuus, lakini juhudi zetu zimeishia ukingoni, nasi hatukuweza kupata ithibati yeyote ili kuhusiana na sentensi ...
Neno Tharu-Llahi (ثار الله) limekuja likiwa na maana mbili: moja ni kwa maana ya damu, na ya pili ni kwa maana ya kulipiza kisasi na kutaka kummwga damu ya muuwaji. Kwa hiyo maana ya mwanzo inapotumika kwa ajili ya kumuita Yeye (a.s) Tharu-Llahi (
Ufafanuzi juu ya swali lako ni kwamba: jua ni moja kati ya vitu vyenye kutoharisha, na miongoni mwa vitu vyenye kutoharishwa na jua ni: ardhi pamoja na kuta za nyumba.[i] Ili jua liweze kutoharisha ardhi na pamoja na zile kuta za nyumba ...
Rejeo mama na asili hasa zinazo aminika ambazo zimeyanukuu maandiko ya Sala na salamu (Ziara) za siku ya Ashura ni vitabu viwili, navyo ni: kitabu Kaamiluz-ziaaraat cha Jaa'far bin Muhammad bin Quulewaihi Qummiy, ambaye amefariki mwaka 348 Hijiria, na cha pili ni kitabu kiitwacho Misbaahul-mujtahid cha ...
Ayatu-Llahi Mhdi Hadawiy Tehraniy (Mungu Amhifadhi), amelijibu swali hili kwa kusema: Bila shaka Maimamu (a.s) ni wenye mamlaka kamili ya kuitawala na kuzisarifu za waumini, lakini kufanya hivyo huwa kunahitajia idhini ya Mola Mtukufu, hivyo basi wao (a.s) huwa hawafanyi hivyo isipokuwa kuwe na maslahi maalumu juu ...
Uislamu umekuja kwa ajili ya kuwapangia wanaadamu mfumo maalumu wa sheria za kijamii, sheria ambzo ni kwa ajili ya kuweka uhusiano salama na wenye mafanikio baina yao wenyewe kwa wenyewe, baina yao na Mola wao na baina yao na viumbe vyengine vilivyo hai na visivyo hai ulimwenguni. ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...