Imamu Husein bin Ali (a.s) ambaye ni Imamu wa tatu wa Kishia, ni mtu mwenye fadhila kubwa mbele ya Mola wake, na fadhila hizo amezipata kwa kutokana na malengo yake, matendo, kutojitanguliza mbele katika maslahi ya jamii yake pamoja na kule kujitoa keake muhanga kwa ajili ya ...
1- Suala la Malaika kuumbwa kutokana na nuru ya watu fulani, ni suala maarufu lilinukuliwa kutoka kwenye Riwaya za pande zote mbili, za Masunni na Mashia. Ndani ya vitabu vya Kishia, kuna Riwaya zinazoelezea kuwa: Malaika wameumba kutokana na nuru za watu maalumu, kama vile: Mtume na ...
Namna ilivyotumiwa Aya iliopita hapo juu ambayo ni (Aya ya 13 ya Suratu Sijda) katika usimamishaji wa dilili hiyo iliyosema kuwa: Mola hakuwaongoza viumbe wake, haikuwa sawa. Kwa sababu ni wazi kabisa kuwa; ukweli uko kinyume na usemi huo, kwani Mungu Mtukufu anamtakia kila mmoja kheri na ...
Ndani ya Qur-ani na Riwaya mbali mbali, kuna mafunzo mbali mbali yenye kuwafahamisha waja masharti ya mwanzo yanayosababisha kukubaliwa amali zao, na masharti msingi yaliyotajwa katika mafunzo hayo ni kumuamini Mola, kujiepusha na shirki pamoja kuto ritadi, na bila ya kuwepo misingi hiyo Mola hatozikubali aina zozote ...
Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
Neno Tharu-Llahi (ثار الله) limekuja likiwa na maana mbili: moja ni kwa maana ya damu, na ya pili ni kwa maana ya kulipiza kisasi na kutaka kummwga damu ya muuwaji. Kwa hiyo maana ya mwanzo inapotumika kwa ajili ya kumuita Yeye (a.s) Tharu-Llahi (
watu kama hawa wanatakiwa kusali safari, na pia hawaruhusiwi kufunga katika hali kama hiyo, na wala hawawezi kufunga funga zao za nadhiri huku wakiwemo ndani ya mwezi wa Ramadhani tena safarini. Lakini iwapo wao wataifikia sehemu walioikusudia kwenda kubaki hapo kabla ya kukengeuka kwa jua, ...
Mtu atakaeingiliwa na usiku wa Idil-fitri, huku akiwa ni baleghe na mwenye akili timamu, naye akiwa si mtumwa wa mtu wala si fakiri, mtu huyo atawajibika kutoa zakatul-fitri kwa ajili yake na kwa ajili ya wale wote anaowahudumia, na kiwango cha kila mmoja ni kiasi cha kilo ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...