advanced Search
KAGUA
7696
Tarehe ya kuingizwa: 2012/03/15
Summary Maswali
je hivi kuna kifungu chochote kile ndani ya sheria ya kiislamu, chenye kuzungumzia suala la mtu kuwa na kazi mbili tofauti? Na je suala la mtu kuwa na kazi mbili tofauti, huwa linaanisha kuwa mtu huyo ni mwenye kuiendekeza au kuipenda sana dunia kuliko Akhera?
SWALI
je kuna aina yoyote ile ya fatwa au hukumu kuhusiana na mtu kuwa na aina mbili mbali mbali za kazi, au kushika aina mbili za madaraka kwa wakati mmoja? Na je kufanya hivyo huwa kunaonesha kuwa mtu wa aina hiyo ni mwenye kuyapenda zaidi maisha ya kidunia kuliko yale ya Akhera? Tafadhalini naomba muongozo weno.
MUKHTASARI WA JAWABU

Kwa kweli kisheria hakuna matatizo yoyote yale kuhusiana na suala hilo la mtu kuwa na aina mbili za kazi au madaraka. Ndio Uislamu umewatahadharisha watu kuhusiana na kuwa na mapenzi makubwa ya kuipenda dunia na kuyasahau maisha ya Akhera, dlakini mtu anaweza akawa na aina mbili za kazi huku yeye pia akawa ni mcha Mungu, na kwa upande mwengine, yawezekana mtu akawa na kazi na madaraka mamoja tu, lakini yeye akawa ni mpezi wa maisha ya kidunia kupita budi. Hapa sisi tunaweza kusema kuwa: wakati mwengine huwa ni jambo la wajibu na lazima mtu kuwa na madaraka au shughuli za aina mbili, kwani wakati mwengine kipato anachokipata kutoka katika kazi yake, huwa hakiwezi kukidhi mahitajio ya maisha yake ya kibinasi na kifamilia, katika hali kama hii hii basi mtu huwajibikiwa kutafuta kazi ya pili kwa ajili ya kukidhi mahitajio hayo.

 

 

Kwa upande wa sheria na kanuni serikali ndani ya jamii mbali mbali, kila nchi huwa na hukumu yake ya kisheria kuhusiana na swali lako hili, lakini pia tunatakiwa kufahamu kuwa: suala la mtu kushika aina mbili za madaraka, linaweza kumsababishia yeye kutoweza kuzitekeleza kazi zake kimakini na kikamilfu. Na wakati mwengine kule mtu kuwa na kazi mbili kunaweza kumsababishia yeye asiweze kumudu kisawa sawa kazi zake za msingi, kama vile kazi za malezi na kuishughulikia familia yake kisawa sawa, katika hali kama hiyo yeye hatoruhusiwa kushika kazi na nyadhifa za aina mbili. Hii inatokana na kule shria kuyazingatia maniufaa kamili ya mwanaadamu kibinafsi na kijamii, kwa hiyo sheria haiwezi kumvumilia mtu anayevuruga maslahi msingi ya maisha yake au jamii yake kwa utashi wa kujitafutia maslahi bora zaidi yasiyo ya msingi kama vile kipato au madaraka na uluwa. Kwa kutokana na kuwa, kigezo bora na madhubuti kwa wanaadamu ni Mtume wetu Muhammd (s.a.w.w), hebu basi tuiangalie Riwaya kutoka kwa Imamu Husein (a.s) aliyoipokea kutoka kwa baba yake Ali (a.s), Yeye (Imamu Husein (.s)) Amesema: (Mimi nilimuuliza baba yangu kuhusiana na maisha ya Mutme (s.a..w.w), Naye (a.s) akaniambia: Yeye Mtume (s.a.w.w) alikuwa akirudi nyumbani kwake kwa hiyari yake mwenyewe na hakuwa akisukumwa na au kuvutwa na mtu fulani, Naye (s.a.w.w) alikuwa akiugawa wakati wake sehemu tatu: sehemu moja ni ya ibada, sehemu ya pili ni ya familia yake na sehemu ya tatu ni yake yeye…)[1]

 


[1] Ibara ya Hadithi hii kwa lugha ya Kiarabu ni kama ifuatavyo:

"قال الحسين عليه السّلام: سألت أبي عن مدخل رسول اللّه صلّى اللّه عليه و آله، فقال: كان دخوله في نفسه مأذونا في ذلك، فاذا آوى إلى منزله جزّى دخوله ثلاثة أجزاء: جزءا للّه و جزءا لأهله و جزءا لنفسه ..."

Tarjama ya Sunanun-Nabiy, cha Allaama Tabaatabai, juz/1, uk/15 na 19, ya Muhammad Hadi Faqhiy, chapa ya saba ya Kitabu Furuushiy Islaamiyya, Tehran, mwaka 1378 Shamsia.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
  4839 تقلیدچیست؟
  Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku. Katika hali yakawaida, ...
 • Je ni kweli kuwa Imamu Husein (a.s) aliwahi kuwa na binti mwenye umri wa miaka mitatu au mine, aliyejulikana kwa jina la Ruqayya au Sukaina anaye semekana kuwa alifariki dunia huko Damascus?
  6601 اهل بیت و یاران
  Ingawaje wengi miongoni mwa waandishi wa Historia hawakukinukuu kisa cha kuwepo kwa mtoto huyo wa kike wa Imamu Husein (a.s) mwenye umri wa kiasi cha miaka mitatu au mine, aliyejulikana kwa jina la Ruqayya au Fatimatu Sughra na baadhi ya wakati akijulikana kwa majina yasiokuwa hayo, lakini ...
 • kwa mtazamao wa Kiislamu, mwanaadamu ni kiumbe gani?
  8466 Elimu mpya ya Akida
  Kwa mtazamo wa Qur-ani, mwanaadamu ni kiumbe aliyebeba sifa mbili tofauti za kimaumbile, moja ni ile inayotokana na maumbile aliyopewa tokea mwanzo kutoka kwa Mola wake, nayo ni maumbile ya kiroho, na ya pili inatokana na maumbile ya kiwiliwili alichonacho. Maumbile asili ya kiroho (kifitra), huwa ni ...
 • Qur-ani ni muujiza wa mtume wa mwisho (s.a.w.w), muujiza wake basi uko katika hali gani?
  7770 Elimu za Qur-ani
  Kuna hali tatu za kimiujiza zilizotajwa kuhusiana na muujiza wa Qur-ani: muujiza unaohusiana na maneno ya Qur-ani, muujiza wa yale yalioomo ndani yake na muujiza wa Yule aliyekuja na Qur-ani (s.a.w.w) Muujiza unaohusiana na maneno ya Qur-ani umegawika katika sehemu mbili:
 • kuna tofauti gani baina ya tabia na eimu ya tabia (saikolojia)?
  24451 Tabia kimtazamo
  Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
 • Shin aure yana da wasu sharaDai na musamman?.
  2522 Sheria na hukumu
  A mahangar musulunci auren da’imi da na mutu’a suna da sharaDai waDanda sune kamar haka:- 1. Karanto siga (Yarjewa juna tsakanin miji da mata shi kaDai bai wadatar ba lalle ne a hada shi da furta “farar da” lafazi na musamman). 2. Bisa ihtiyaDi na wajibi ya ...
 • je ndani ya hadithi kuna ushahidi wowote unaoelezea kuwa Ramadhani ni siku tahalathini?
  7405 Elimu ya Hadithi
  Kila mwaka wa Hijiria kwa kawaida huwa una miezi kumi na mbili, na masiku ya miezi huwa yanahesabiwa kwa kuonekana kwa mwezi, hii ni kanuni ya mwaka wa Hijiria, ama mwaka Shamsia kwa kawaida masiku yake huwa tayari yameshatambulikana, na suala la kuonekana kwa mwezi si suala ...
 • kuna dalili yoyote ile inayothibitisha kuwa Shimru alimchinja Imamu Husein (a.s) kwa kisogoni?
  4866 حوادث روز عاشورا
  Suala hilo limenukuliwa kutoka sehemu tofauti: 1- Imenukuliwa katika maneno ya Zainab (a.s) yaliyosema: “Ewe Muhmmad (s.a.w.w), wanao wa kike wamefanywa kuwa ni mateka, na wanao wa kiume wameuwawa, na upepo unavuma juu ya miili yao, na huyo hapo Husein (a.s) yupo chini hali akiwa ...
 • je mwenye saumu anaruhusiwa kukoga janaba?
  15678 جنابت
  Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
 • Timsahın saxlanılması və digər ölkələrə satışına icazə varmı?
  4436 دیگر آبزیان
  Təqlid olunan müctehidlərin cavabları bunlardır: Həzrət ayətullah Xamnei (Allah qorusun) Əti haram olan heyvanların saxlanılması və onun hətta, bu heyvanların ətlərinin yeyilməsini halal bilənlərə də satılması düzgün deyildir. Amma, aqillər nəzərində halal mənfəətə görə olsa məsələn, ətinin başqa ət yeyən heyvanlar üçün istifadəsi yaxud, dərisinin dəri sənətində ...

YALIYOSOMWA ZAIDI