advanced Search

بلاگ

Ingawaje yawezekana upotoshwaji uliopatikana ndani ya Taurati na Injili ilioko mikononi mwa waumini wa Kikristo, ukawa umeyafuta majina ya watukufu hao, [1] lakini bado kuna Hadithi zenye kuelezea kuwa majina hayo yalikuwa ni maarufu ndani ya vitabu hivyo, nao walikuwa wakijulikana kwa jina la Aalu Abaa (a.s), na ibara hii ilikuwa ikiwakusudia:

Kwa mujibu wa nukuu za baadhi ya Hadithi ni kwamba, majina ya matano ya Aali Abaa (a.s), yaani Aali wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambao ni: Ali, Fatima,Hasan na Husein, yametajwa ndani ya Taurati na Injili. Pia suala hilo linaonekana kuashiriwa ndani ya ile Hadithi yenye kunukuu majadilianao ya kielimu yalipita baina ya Imamu Ridha (a.s) na watu wawili, ambao ni Jaaliith ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Kanisa, na Ra-asul-Jaaluut ambaye ni miongoni mwa wakuu wa Kiyahudi.

thawabu za aiara ya Imamu Husein (a.s)

Jumanne, 25 Agosti 2020

Uislamu ni dini ya matendo, na malipo ya matendo hayo yapo kwa Mola mwnyewe, na ujira bora zaidi juu ya matendo hayo humuangukia yule mwenye matendo yaliotimia zaida kiikhlasi, na Mola ndiye mlipaji bora kuliko walipaji wote, naye hatoupoteza ujiwa wa mtu yoyote yule miongoni mwa watendaji hao.[1] Kila nia ya mja juu ya matendo ayatendayo inapokamilika kiikhlasi, na kila mja apostahamili madhila na mitihani mbali mbali kwa ajili ya Mola wake, ndipo anapopata ujira mkubwa zaidi, na thamani yake huwa ni kubwa zaidi mbele ya Mola wake. Na msingi huo ndio uliowafanya mitume na Maimamu (a.s) kuwa na cheo kikubwa zaidi kuliko wengine mbele ya Mola wao. Imamu Husein naye (a.s) ambaye ni Imamu wa tatu wa Kishia, ni mtu mwenye cheo kikubwa mbele ya Mola wake.

Hongera kwa kuzaliwa kwa Imam kazem (as)

Jumatatu, 10 Agosti 2020

Hongera kwa kuzaliwa kwa Imam Hadi (as)

Jumanne, 04 Agosti 2020

Kwa mara ya kwanza kabisa tovuti ya Islamquest ilianza kazi yake mnamo tarehe 2/4/2006, ambapo tovuti hii ilianza kutoa huduma zake kupitia lugha ya KIpashia, Kiarabu na Kiingereza.
   Lengo hasa la kuanzishwa kwa tovuti hii, ni kubeba jukumu la kujibu maswali mbali mbali yanayohusiana na dini ya Kiislamu kupitia njia ya mtandao wa internet.
Toleo la kwanza la tovuti hii liliweza kukamilika chini ya juhudi kubwa zilizofanywa na kikundi cha vijana mahodari wenye misingi madhubuti ya dini waliojitolea kuitekeleza kazi ya uundaji wa tovuti hii.
 

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI